a

Je, ungependa kuwa na washirika wa uhakika nyumbani na nje utakaoweza kufanya nao shughuli mbalimbali kwa ajili ya maendeleo yako wewe, ndugu na rafiki zako?

 

Mimi naitwa Michael T. Mwakilasa, mzaliwa wa Kyela, Mbeya kwa sasa ninaishi Jersey City, New Jersey, nafanyakazi New York City, New York. Mwenyezi mungu kanijaria kupata mke na watoto wawili wa kiume.

                           

Nimeishi Canada miaka mitatu, nikaishi Marekani miaka 7 nikarudi nyumbani ambako nilikaa miaka mitatu na sasa nipo hapa Marekani miaka sita. Ninazungumzia haya yote ya kubadlilisha makazi ili uelewe jinsi nilivyoishia kuanzisha hii tovuti.

Kwanza kabisa, kutokana na mimi kuzaliwa kwenye familia ya kawaida nimeanza kufanya biashara ndogo ndogo na huku nasoma tangu nikiwa sekondari. Nilipomaliza elimu yangu ya chuo nikaendelea na biashara ndogo ndogo.Niliondoka nyumbani kwenda nje kutafuta mtaji wa kuendeleza kibiashara changu, baada ya miaka kama kumi hivi nje, miaka ya kutumwa sana nilirejea nyumbani ili  nifanye biashara zangu, lakini baada ya miaka mitatu ilinibidi niondoke tena nyumbani na kuja nje kwa ajiri ya kutafuta nguvu mpya!!!!

Tatizo langu kubwa nililojifunza katika kuhangaika kwangu ni kutokuelewa hali halisi ya nyumbani ilivyokuwa na kutokuwa na washirika wa uhakika. Maana yangu ni kwamba, nilipoondoka nyumbani baada ya muda mrefu mawasiliano yangu makubwa na nyumbani Tanzania yalikuwa ni kwa wazazi wangu na ndugu zangu wakaribu, rafiki zangu nilikuwa nazungumza nao siku moja moja. Nilipokuwa nataka kufanya mradi wowote ilinibidi niwatumie hao ndugu zangu, lakini hawakuwa na udhoefu wowote na shughuli nilizotaka kufanya kwahiyo hatimaye hazikufanikiwa. Niliporudi nyumbani nikaanza kufufua mtandao wangu, nikaandika kitabu cha kumuhenzi baba wa Taifa alipofariki Tanzania Tutakukumbuka milele Baba wa Taifa na shughuli ndogo ndogo za kuuza vitu Marekani, nikakwama kidogo kuhusu soko kwani nipokuwa naishi Marekani sikutafuta soko kwani nilikuwa natumwa tu, na watu wote niliotaka ninaowafahamu wanaoishi Marekani niliotaka kufanya nao wanakimbizana na ajira ya masaa, hawana muda wa kufanya miradi.

Baada ya kupata fundisho hili, Katika miaka minne sasa nimekuwa natafuta masoko na jinsi ya kuuza bidhaa za Tanzania nje na kujenga mtandao na washirika mbalimbali wa uhakika katika nyanja zao walizosomea au wanazofanyia kazi, wengine nimesoma nao, tumekua pamoja, nimekutana nao katika kusafiri, au watu wa uhakika wameniunganisha, wengine nimekutana nao kwenye mtandao wa internet.

Nadhani kwa wewe kutonifahamu mimi siajabu unadukuduku kujua nina nia gani? Kutokana na mafanikio madogo niliyopata nia yangu kubwa ni kuzidi kuongeza mtandao wangu. Mimi leo nimefika hapa kutokana na watu wengi waliochangia katika maisha yangu toka nipo mdogo, Kuna jamaa mmoja hapa New York amefanikiwa sana katika biashara zake, aliulizwa nini siri yake ya mafanikio akajibu "Kama ukiweza kuwasaidia watu wengi waweze kufanikiwa, na wewe utafanikiwa". Naamini kabisa kuna watanzania wenzangu wengi wenye matatizo kama yangu na tukishirikiana sote tutanufaika.

Tafadhali tutembelee kwenye tovuti zifuatazo:

 

www.mtukwao.com

www.sisikazi-economic-empowerment-centre.org

www.best-tanzania-travel-guide.com

 

Naomba tuanze kujuana kwa kujiandikisha gazeti pepe la kila mwezi na kubadilishana mawazo kwenye baraza.

  

Jiandikishe kupokea  Gazeti-pepe la kila mwezi
Jina la lako
(muhimu)
Jina la ukoo
Barua-pepe
(muhimu)

 

 

 Rudi Maskani

Do you like this website? Tell your friends about it!