Baishara na Fedha ni uti wa mgongo wa hii tovuti. Nadhani kuna tovuti nyingi tu za watanzania zenye kuzungumzia mambo mbalimbali ya jamii. Sisi tujaribu kuzungumzia zaidi jinsi ya kuweza kubadilisha maisha yetu katika biashara za ujenzi wa nyumba za kuishi na kupangisha, kununua hisa kwenye makampuni, kuanzisha biashara, kufanya biashara za kimataifa.
Mimi naamini kabisa sisi watanzania tunaoishi nje tuna nafasi kubwa sana ya kuendelea sisi wenyewe na jamii zetu nyumbani. Tukijitahidi zaidi na kuweza kujifunza wenzetu wanavyofanya vitu vyao tutaendeleza nchi yetu kwa ujumla.
Watanzania wanatuma nyumbani dola milioni 50 na chengi kila mwaka, Bofya hapa. Wenzetu waganda watuma milioni 400 na chengi. Kutokana na uchunguzi wa ILO-suported East African Labour Migration Project, watanzania wako tayari zaidi kuwekeza nchini licha ya matazizo tuliyokuwa nayo. Wakati muafaka umefika wa kukusanya nguzu na kufanya vitu vya uhakika, tafadhali bofya hapa.
Nipeleke Dukani
Nirudishe Maskani